Home Entertainment Kesi ya Lulu kumuua muigizaji Kanumba yaanza kusikilizwa upya.

Kesi ya Lulu kumuua muigizaji Kanumba yaanza kusikilizwa upya.

393
0
SHARE
Katika picha. Muigizaji (Lulu) Elizabeth Michael. wakati akitokea mahakamani.
Inaripotiwa na (Shaaban) kutoka simamia.com

Kwa Ufupi: Mahakama Kuu ya Tanzania inatarajia kuendelea kusikiliza ushahidi wa kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, October 20, 2017.

simamiateam@gmail.com

Dar Es salaam. Lulu anadaiwa kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake marehemu Steven Kanumba, April 7, 2012 nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican, DSM.

Leo October 19, 2017, kesi hiyo imeanza kusikilizwa ushahidi kwa mara ya kwanza, ambapo ushahidi umetolewa na mdogo wa Kanumba, Seth Bosco mbele ya Jaji Sam Rumanyika.

Muigizaji: Stiven C. Kanumba enzi za uhai wa mwili. ~picha na maktaba simamiaMediaGroup~

Katika ushahidi huo, Bosco aliongozwa na Wakili wa serikali, Faraja George, huku Lulu akiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala.

Katika ushahidi wake Bosco ambaye alikuwa akiishi na marehemu maeneo ya Sinza, aliieleza mahakama jinsi simu ilivyosababisha ugomvi baina ya Lulu na Kanumba hadi kupelekea umauti wake.

Baada ya kutoa ushahidi huo, Jaji Rumanyika ameahirisha kesi hiyo hadi October 20, 2017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Kwa habari hii una maoni gani?? Tuandikie hapo chini kwenye comment.