Home News Ufaulu kufikia asilimia 80

Ufaulu kufikia asilimia 80

259
0
SHARE
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa

BAADA ya kupata mafanikio katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imedhamiria kuongeza kiwango cha ufaulu kwa shule za msingi na sekondari, kutoka asilimia 70 hadi 80 mwaka huu.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa aliyasema hayo jana Dar es Salaam, wakati wa mkutano maalumu wa wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, kuhusu utekelezaji na mafanikio ya BRN.

Dk Kawambwa alisema, wakati mpango huo ukianzishwa mwaka 2012, wizara hiyo ilijiwekea ufaulu kwa shule za msingi na sekondari uwe asilimia 60 kutoka asilimia 31 kwa shule za msingi, na kutoka asilimia 42 miaka ya nyuma kwa shule za sekondari.

Alisema kuwa wizara ilifanikiwa kuhakikisha ufaulu wa kufikia asilimia 50.1 kwa shule za msingi na asilimia 58 kwa shule za sekondari. Dk Kawambwa aliwahakikishia wafanyakazi wa wizara hiyo pamoja na taasisi zilizo chini yake kuwa, kama wataendelea kujituma kama walivyofanya chini ya uongozi wake, wizara hiyo itaendelea kuongoza katika BRN.

Alisema, mafanikio mengine waliyoyapata chini ya mpango huo ni kuweka uwazi katika matokeo, kutoa motisha kwa shule ambazo zimefanya vizuri, kusaidia maeneo yenye uhitaji zaidi na kuboresha hali za walimu.