Home Entertainment Shilole Afunguka Alichopewa na Mchumba ake

Shilole Afunguka Alichopewa na Mchumba ake

76
0
SHARE
MKALI wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Zuwena Mohamed ‘Shilole au Shishi Baby’ anadaiwa kubondwa na mpenzi wake wa sasa anayejulikana kwa jina moja la Uchebe, kisa kikisemekana ni wivu wa kimapenzi.

Chanzo makini kililiambia Ijumaa Wikienda kuwa, hivi karibuni Shishi alikwenda kwenye shoo mkoani Morogoro akiwa na Uchebe, akiwa jukwaani shabiki alipanda na kumshika kimahaba, alipomaliza shoo ndipo mchumba’ke huyo akamshushia kipigo.

Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Shishi ambaye alifunguka:

 “Ni kweli kulitokea mgogoro wa kawaida, ilikuwa Zanzibar na siyo Morogoro. Unajua jamaa hatumii kilevi, sasa mimi nilimkwaza kwa sababu nilitaka kuendelea kunywa ndiyo tukapishana kauli.

Kuhusu wivu ni kweli anao na huyu ni mwanaume nampenda sana siyo kama wengine waliopita,” alisema Shishi anayekimbiza na ngoma yake mpya ya Kigori.

TOA MAONI YAKO