Home Business Ndege Zisizo na Rubani Kusambaza Dawa Nchini Tanzania.

Ndege Zisizo na Rubani Kusambaza Dawa Nchini Tanzania.

831
3
SHARE
Mkurugenzi Mtendaji wa Zipline Keller Rinaudo akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa(MSD) Laurean Bwanakunu.
kutoka simamia.com na (Shaaban)

Kwa ufupi:
Ni mara ya kwanza kutolewa kwa huduma hiyo hapa nchini.

simamiateam@gmail.com

Dar es Salaam. Serikali, Bohari ya Dawa (MSD) kwa kushirikiana na kampuni ya Zipline kutoka nchini Marekani wamesaini mkataba wa makubaliano ya kusambaza dawa kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani ‘drones’.
Tukio hilo lililofanyika katika ukumbi mdogo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya afya waliohusika katika utafiti uliochukua miaka mitatu wakiwemo Ifakara Health Institute (IHI).
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa MSD Lauren Bwanakunu amesema makubaliano hayo yataanza rasmi mara moja kuangalia namna ya kuanza kutumia teknolojia hiyo.
“Wenzetu wa Ifakara watafanya utafiti kuangalia uwezekano wa drones kufanya kazi Dodoma na Mwanza wakipata matokeo chanya tutaanza kusambaza dawa kwa kutumia Ndege hizi,” amesema Bwanakunu.

Tuandikie Maoni yako hapo chini kwenye comment.

3 COMMENTS

  1. HUOM-PANGO WA KUSAMBAZA DAWA KWAKUMIANDEGE ZISIZO NA RUBANI NI M-PANGO MZUL WA KIMAENDELEO JE ! NDEGEHIZO ZITATUWA HATA VIJIJINI KWA WADAUWENGI ? KAMA NDIVYO NIMPANGOMZULI

  2. Issue yetu kwanza ni upatikanaji wa hizo Dawa, hizo Ndege hats kama ni za bure, bado siyo busara kuomba aina huyo ya msaada, bado dawamuhimu ktk mahospitali ya umma ambako ndiko watu maskini wanako tibiwa hazipatikani kikamilifu. Dawa nyingi zimejaa kwenye hospitality za kulipia. Ndege zitakuwa zinapeleka Dawa gani huko?

  3. Itakua vizuri maana dawa zitafika kwa wakati

    Na hii isiwe kwenye dawa tu iwe hata kwenye huduma nyingine muhimu ili watu wazipate huduma hizo kwa wakati

Comments are closed.