Home Latest News Fahamu, Kati ya pin na Password kipi bora Android, IOS #Usalama.

Fahamu, Kati ya pin na Password kipi bora Android, IOS #Usalama.

147
0
SHARE
Picha katika ulinzi wa screen ya sim. pin na pattern.
Inaripotiwa na (Shaaban) kutoka simamia.com

Kwa ufupi: Ufunguaji wa simu wakati ikiwa imelokiwa ulikua ni rahisi sana hapo mwanzo, lakini kumbuka kuwa ilikua ni rahisi vile vile kuweza kuibiwa taarifa zako kwani mtu angeweza kufungua kifaa chako kwa urahisi.

simamiateam@gmail.com

Dar Es salaam. Teknolojia imekua na vilevile simu zetu zinahifadhi karibia kila kitu chetu mpaka vile vya siri. Je, ni njia gani ya msingi ya kuitumia kati ya ‘Pin au Pattern’ ili kujihakikishia usalama wa hali ya juu?
Simu nyingi za zamani kama vile Nokia na zingine ilikua inakuladhimu kubonyeza vitufe viwili kwa haraka ili kuweza kufungua simu hiyo (menyu na nyota). Lakini vipi kwa simu za kileo (simu janja), hapa ndipo habari nyingine inapokuja.

Pin na pattern’s jinsi ya kufungua loki ya sim yako kwa pin vs patterns.

iOS Vs. Android.​

Apple kwa mara ya kwanza walianzia teknolojia ya ‘Slide to unlock’ ambayo Steve Jobs mwenyewe alisema ni njia rahisi ya kuzuia simu kujipiga au kujibonyeza yenyewe pindi ikiwa mfukoni mwa mtu. Vilevile Apple walikua na jinsi ambavyo mtumiaji wa vifaa vyake anaweza kuweka loki (maarufu kama passcode) kwa kutumia pin nne (Sasa anaweza hadi kuweka pin sita).

​Android​
Tukija kwa Android njia maarufu ya kuweza kutoa ulinzi (lock ) katika simu ni kwa kutumia ‘Pattern’ ambapo njia hii inasemekana sio ya kuisalama sana kama vile watu wanavyofikiria. Yaani kati ya kutumia Pin na Pattern ni bora mtumiaji wa Android atumia Pin ili kujihakikishia usalama wa hali ya juu.
Wataalamu wa ulinzi na usalama wa Marekani, Naval Academy wamefanya utafiti ambao umebainisha hilo pamoja na kushirikiana na chuo kikuu cha Maryland Baltimore County. Katika utafiti huo iligundulika kuwa ni rahisi sana kushika Pattern za simu ya mtu pindi akiwa anafungua simu yake kuliko yule ambae anatumia Pin.

​kitu cha Kufanya​
Kama ni mtumiaji wa Android, fanya juu chini uachana na kutumia ‘Pattern’ na uhamie katika ‘Pin’ tena utumie zile zenye tarakimu sita kwa usalama zaidi. Lakini vilevile labda dunia inapokwenda sasa hivi kutakua hakuna haja tena ya kuwa na ‘Pattern’, kwa sasa simu zinatolewa loki kwa kutumia alama za vidole vile vile hata kwa uso (iPhone X).
Nipe.

Nipe mawazo yako hapo chini sehemu ya comment. hivi ni mara ngapi umebadilisha password yako kisa tuu mtu kaiona na hukutaka haijue.!