Home Latest News Raia wasio watanzania kunyanganywa Aridhi wanazomiliki hapa Tanzania.

Raia wasio watanzania kunyanganywa Aridhi wanazomiliki hapa Tanzania.

1546
0
SHARE

kutoka-simamia.com

SERIKALI imesema watu wasio raia na wenye hati mbili za kusafiria watanyang’anywa ardhi wanayomiliki kama ilivyo kwa wale ambao hawaendelezi ardhi wanazozimiliki.Hayo ameyabainisha jana wakati wa kuhitimisha mjadala wa Taarifa ya Hali ya Uchumi 2016 na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/18 iliyowasilishwa bungeni Juni 8, mwaka huu, ambayo jana Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alihitimisha mjadala huo na wabunge kuipitisha kwa kura ya wazi.“Tutaendelea kufanya ukaguzi kwa sababu tunafahamu katika suala la uwekezaji kuna matapeli wa kuchukua ardhi ya Tanzania kwa ajili ya kujipatia mitaji na kuhamisha mitaji, wanatumia ardhi yetu kufanya mogeji na kujipatia fedha,” alieleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.“Kwa hiyo, tunafanya ukaguzi kuwatambua wale wote waliopewa ardhi na hawana sifa, wasio raia na wanaomiliki bila kuendeleza. Tunajua kuna watu wamemiliki hata ardhi yenye madini kwa sura za kitanzania na hati za kitanzania, kuna wengine wana hati mbili mbili, kwa maana wana uraia wa nchi mbili, uhakiki utagundua wana hati mbili mbili na wanamiliki ardhi tutawanyang’anya kama tulivyowanyang’anywa watu wengine, wakati wa longolongo umekwisha sasa,” aliongeza Lukuvi.“Kwa mwaka huu wa fedha, Rais Magufuli amefuta hati za mashamba zaidi ya 20,000 mkoani Morogoro, sambamba na mashamba ekari 100,000 maeneo mengine na kuwa sasa utaratibu unafanywa kugawiwa kwa wananchi”. Kuhusu uwekezaji wa mradi wa mtambo wa kuchakata gesi huko Lindi wa LNG, Lukuvi alisema tayari wizara imeshatoa hati ya eneo lote kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), hakuna tatizo la ardhi.Kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta, Lukuvi amewaonya wananchi ambao wanajenga vibanda vya miti kwa lengo la kujipatia fidia, kuwa serikali haitatoa fidia kwa watu hao kwani wameshapiga picha ya anga. Alisema pamoja na hilo, pia imepunguza tozo ya umilikiaji wa ardhi kwa asilimia 67, lengo ni kuwafanya wananchi wengi wamiliki ardhi na serikali inapata mapato.“Mwaka huu wa fedha tumeamua kuondoa gharama za umilikaji wa ardhi asilimia 67 ya tozo kubwa iliyokuwa ikiwakwaza wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, inayoitwa ‘premium’, mfano ulitakiwa kulipa Sh milioni 100 sasa kuanzia Julai utalipa Sh milioni 33, lengo ni kutoa unafuu wa watu wengi kuweza kumiliki ardhi.Kwa wananchi wa Dodoma, alisema wameanza kutoa hati ya miaka 99 na kuwa wale waliopewa ofa za miaka 33 wataongezewa miaka 66 na kuwa watapewa hati bure. Tumerahisisha na kuondoa viwango katika ardhi, zamani ili kupata hati lazima upate ndani ya mwaka mmoja, lakini sasa tumeweka mfumo katika Wilaya ya Ubungo na Kinondoni, tumeanza kuscan nyaraka mbalimbali tutaanza kufikia mwakani tukifunga mitambo hii nchini,” alieleza.