Home Latest News Oparation Ilivyokuwa hadi kumpiga risasi Osama Bin Laden.

Oparation Ilivyokuwa hadi kumpiga risasi Osama Bin Laden.

437
2
SHARE
kutoka simamia na (Shabaan)

Tangu kuuwawa kwa Kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda Osama bin Laden…

kumekuwa na fununu nyingi
zinazoeleeza mazingira ya kifo chake
pamoja na ujumla wa maisha yake
wakati akiwa mafichoni.

Akiwa mtu mwenye tabasamu na
ucheshi wa mbali, askari (jina
linahifadhiwa) anatoa maelekezo
kwa mwandishi wa habari aliyetaka
kujua historia ya maisha yake
jeshini. Ndani ya mgahawa
uliofurika watu waliochangamka kwa
vinywaji, askari mwanamaji anaanza
kueleza namna alivyojiunga na Jeshi
la Wanamaji la Marekani hadi
kufikia nafasi ya kuwa mlenga
shahaba mkuu.

Anasema anakumbuka kile
kilichomsukuma kuchukua uamuzi
wa kujiunga na jeshi ni kama sehemu
ya hasira iliyomkumba baada ya
kuachwa na mpenzi wake al iyedumu
naye kwa kipindi kirefu.

Unajua tukio la kuachwa na mpenzi
wangu lilinivunja moyo sana… na
ndiyo nikachukua uamuzi kwenda
jeshini.

Anasema kuwa siku yake ya kwanza
alipokwenda kuomba kazi
anakumbuka alimwambia ofisa
mmoja wa jeshi kuwa alikuja hapo
kuomba kazi ya kulenga shahaba
(sniper).
Pale nilimkuta askari mfukuzi,
mkufunzi akaniuliza unataka nini…
nikamwambia nataka kuwa mlenga
shahaha, lakini yeye akaniambia
kuwa tayari walikuwa na walenga
shabaha.

Hata hivyo alifaulu kuandikishwa na
baadaye kupelekwa kwenye mafunzo
yaliyimwongezea ujuzi wa kazi na
hatimaye kuungana na vikosi vya
wanajeshi wa maji vilivyosafiri
sehemu mbalimbali duniani. Kama
ilivyo kwa askari wengi wanamaji,
askari huyu alishiriki kwenye
operesheni mbalimbali za kijeshi
ikiwemo zile zilizohusu katika nchi
za Afghanistan na Iraq.

Anasema operesheni yake kubwa ya
kijeshi ilikuwa nchini Afghanistan
ambako vikosi vya Marekani
vilivamia katika eneo hilo katika kile
kilichoelezwa na kukabiliana na
utawala wa Taliban ambao ulitajwa
kuwa na ushirikiano wa karibu na
Kundi la Kigaidi la Al-Qaeda.

Uzoefu mkubwa wa kijeshi niliupata
wakati nikiwa Afghanistan ambako
nakumbuka nilishiriki kikamilifu
kukabiliana na wanamgambo wa
Taliban. Tulipofaulu kuwafurusha
wanamgambo hao tuliendelea
kubakia nchini huko kuimarisha hali
ya usalama na kusaidiana na
wananchi wa eneo lile kurejesha hali
ya usalama.

Kichwa changu kilikuwa tayari
kimeshazoea mizinga na
makombora, maana wakati
mwingine umekaa sehemu ghafla
unasikia kombora linavurumishwa
mbele yako… Ghala nyuma unasikia
mlio wa bunduki.. Kusema kweli
nilijifunza mengi wakati nikiwa
Afganistan.

Wakati huo Marekani ilianzisha
operesheni za kukabiliana na Kundi
la Al-Qaeda ambalo lililodaiwa
kutekeleza tukio la kigaida katika
majengo yake mjini New York na
Washington.

Shabaha ya Marekani ilikuwa
kukabiliana na kiongozi wa kundi
hilo, Osama bin Laden ambaye
wakati huo ilisemekana
amejichimbia mafichoni katika
Milima ya Afghanistan.
Marekani haikuishia kuingia kijeshi
nchini Afghanistan pia iliivamia Iraq
na hatimaye kuuangusha utawala wa
Saadam Husen aliyekuwa akiongoza
Chama cha Baath ambacho kilikuwa
na uhusiano pia na baadhi ya
makundi ya kigaidi.

Anakumbuka kuwa jinsi alivyorejea
nyumbani Marekani na kisha
kuungana na wanamaji wenzio
ambao waliunda kikundi cha
wataalamu wachache walikuwa na
shabaha ya kuleta mageuzi ya
utendaji ndani ya vikosi vya
wanamaji hasa kwa kutumia uzoefu
waliopata wakati wakiwa kwenye
operesheni za kijeshi katika nchi za
kigeni.

Unajua ukishajiingiza kwenye
mambo haya ya kulenga shabaha
hujali tena lolote, wewe unachoona
ni kwamba umeletwa duniani kwa
kazi maalumu na hiyo kazi lazima
uitekeleze kwa wakati uliopangwa,
anasema askari huyo akimwelezea
mwandishi mmoja wa habari namna
alivyoshiriki kwenye kikosi maalumu
kilichoshiriki kwenye operesheni ya
iliyofanikisha kuuawa kwa kiongozi
wa Kundi la Al-Qaeda, Osama bin
Laden.

Kwa masharti ya kutotajwa jina wala
kuonyeshwa picha yake, askari huyo
anasema kuwa, “Tulipomaliza kazi
nchini Afghanistan tulirudi
nyumbani na kuendelea na mazoezi
yetu ya kuogelea katika Ufukwe wa
Miami. Tukiwa kule ghafla tukapata
taarifa baadhi yetu tulihitajika
kwenda Virginia kwa ajili ya kazi
maalumu.

Kusema kweli hatukujua nini
tunachokwenda kukifanya maana
tulielezwa kuwa kuna kazi ya
dharura. Wengi wetu tukabaki
tunahisi labda tunataka kupelekwa
Libya, wengine wakasema labda
tutaenda Japan kukabiliana na athari
za kimazingira baada ya tetemeko
kubwa la ardhi kulikumba taifa hilo.
Katika siku ya kwanza tulivyopata
taarifa, kusema kweli
walitudanganya. Tulizungushwa
maeneo mbalimbali na kila mara
maofisa wetu walikuwa wakitupa
maelezo ya kutia matumaini
wakisema kuwa tusiwe na wasiwasi
tutaarifiwa punde kwani kulikuwa
hakuna jambo lolote la kutisha.

Anasema kuwa baada ya kukaa kwa
siku kadhaa walipelekwa moja kwa
moja hadi yaliko makao makuu ya
upelelezi CIA, ambako walipokelewa
na maofisa wa ngazi juu
aliyewagawanya kwenye vitengo bila
kuwapa maelekezo yoyote.

Wakati tunakwenda tuliambiwa
tungekutana na Waziri wa Ulinzi,
maofisa wa ngazi za juu wa jeshi
pamoja na wataalamu wengine wa
kijeshi. Tulipata hisia jambo
tulioloitiwa huko huenda likawa
kubwa. Tulipofika pale tulikusanywa
kwenye chumba kimoja na baada ya
muda alitokeza mwanamke mmoja
ambaye kwa sura alionekana kuwa
mtu jasiri na mwenye kuelewa kile
anachokizungumza.

Tuliona tumeletewa
televisheni..vifaa vya kivita na
pembeni kulikuwa na ramani kubwa
ambayo hata hivyo ilifunikiwa na
kitambaa . Hatukujua kile
kilichokuwa kinaendelea. Yule
mwanamke aliposimama ndipo
pumzi ikatushuka,” Anaelezea kuwa
walipatiwa maelekezo kuhusiana na
sehemu ambayo inasadikika Kiongozi
wa Al-Qaeda, Osama bin Laden
ndiyo ilikuwa makazi yake.

Yule askari wa kike akiwa katika
hali ya kujiamini, alituonyesha
ramani na kutufafanulia shabaha ya
kuitwa kwenye chumba kile.
Nilishtuka lakini kadiri
nilivyomtazama yule askari
niliamini kile alichokuwa akikisema.
Tulionyeshwa nyumba moja ambayo
iko pekee yake katika eneo la
Abbottabad.

Baada ya hapo tukaingia kwenye
mazoezi makali tukijifunza namna
ya kuingia kwenye nyumba ile na
namna tukavyoweza kumudu
purukushani zozote zinazoweza
kujitokeza.
Mafunzo yetu yalidumu kwa muda
wa wiki kadhaa na kisha tulipangiwa
siku ya kuondoka kuelekea Pakistan.
Anasema kuwa msafara wa kuelekea
Pakistan alianzia nchini Ujerumani
walikoweka kituo na kisha kuruka
moja kwa moja hadi nchini Pakistan
kupitia eneo la Jalalabad.

Unajua wakati tunakatiza anga ya
Pakistan niliingiwa na hofu sana
pengine vikosi vya pale vingeilenga
ndege zetu na kuzitungua maana
kulikuwa hakuna taarifa zozote kwa
Serikali ya Pakistan kuwa Majeshi ya
Marekani yalikuwa yakiingia nchini
humo.

Tulipita eneo lile na hatimaye kufika
Abbottabad. Tulikuwa tumejipanga
vya kutosha. Msafara wetu ulikuwa
na helikopta, ndege za kivita pamoja
na vifaru kukabili hali yoyote korofi
ambayo ingejitokeza.
Nilishangaa kuona kile
nilichoonyeshwa kwenye picha za
satelaiti wakati nikiwa kwenye
mazoezi Marekani ndicho
nilichokishudia pale.

Tulishuka kwenye helikopta haraka
na kisha kuizingira nyumba mara
moja. Kuna wengine walitanda juu
ya paa, wengine madirishani na
wengi walikuwa angani kwenye
helikopta.

Tulipofika mlangoni tulikuta tundu la
risasi, tukashtuka kidogo,
nikamwambia mwezangu acha woga
hebu twende, nikasukuma mlango
hadi ndani.
Wakati kabla hatujaingia ndani
tulisikia sauti ikiita bla, blab la,,,
kumbe ilikuwa sauti ya mmoja wa
walinzi wa Osama ambaye alikuwa
amevalia fulana nyeupe na pajama
nyeupe pia.

Tulimdhibiti na kupanda hadi
ghorofa ya pili ambako tuliwakuta
kina mama wakiwa wanahangaika
na kupiga kelele.
Hatukutaka kuwadhuru tuliwaweka
chini ya ulinzi, nami nikaendelea
kupanda juu hadi ghorofa ya tatu.

Nilipofika chumba cha juu
nilimwona mtu mmoja mrefu kupita
wote, ndevu zake alikuwa ameonyoa
kiasi. Alikuwa ameweka mikono yake
begani kwa mwanamke mmoja
ambaye baadaye nilikuja kugundua
alikuwa mkewe Jamal.
Nadhani alikuwa anafanya vile kama
njia mojawapo wa kujikinga. Alikuwa
amevalia kofia na kuendelea
kuzunguka huku na kule na yule
mwanamke.

Nakumbuka alikuwa mwembamba.
Pembeni yake kulikuwa na silaha
aina ya AK 47, ambayo baadaye
aliishika mkononi.
Binafsi sikutaka kupoteza muda,
nilinyanyua bunduki yangu na
kumiminia risasi mbili usoni na
kisha nikamshudia namna
alivyoanguka chini na kukata roho.

Na huo ndio ukawa mwisho wa Osama kuvuta pumzi ya dunia hii.

Nini maoni yako kuhusu makala hii inayo sisimua tuandikie hapo chini kwenye comment… sambazia na wengine story hii.. simamia Media kwa Habari za Uhakika.

SHARE
Previous articleSHAMSA FORD ALIA NA VIBENTEN
Next articleLipumba kuamia Wabunge wa Majimbo.
Kwa jina anaitwa Shaban Rashid Said Kisleu na ni mhariri hapa Simamia Media Group. Natumaini mtafurahishwa na yake nitakayowaletea na mtaendelea kufatilia mitandao wa Simamia.com Kumfikia, tuma email SimamiaTeam@gmail.com

2 COMMENTS

  1. Marekani walipata shida saana huyu mtu mbona hawakuonyesha picha zake akiwa amefariki. magaidi wengine wakina Gadaf waliwaonyesha wakina Sadam n.k hapa kuna usanii wa kiundishi umetumika kutukonga mioyo tuu.

Comments are closed.