Home Latest News Msako wa Nyumba kwa nyumba kuwasaka wasio na kazi waanza rasimi.

Msako wa Nyumba kwa nyumba kuwasaka wasio na kazi waanza rasimi.

527
0
SHARE
kutoka simamia na (Shaaban)

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke jijini Dsm limeanzisha Operesheni ya nyumba kwa nyumba,Mtaa kwa mtaa wilayani temeke kwa kuwashirikisha wenyeviti wa kamati za usalama za mitaa kufuatia kubaini baadhi ya watuhumiwa wa uhalifu katika eneo hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Giles Muroto akizungumza na wenyeviti wa mitaa na watendaji amesema baadhi ya watuhumiwa wamekuwa wakijificha wilayani humo ili kukimbia msako wa jeshi hilo unaoendelea Kibiti na Rufiji mkoani Pwani.

Aidha, Kamanda Muroto ametangaza Operesheni ya kuwasaka watoto watoro mashuleni wilayani Temeke itakayowashirikisha wenyeviti wa mitaa, ikiwemo wale wasioonekana kwa wazazi wao ambao inadaiwa zaidi ya watoto 1400 hawaonekani shuleni au kwa wazazi wao, hali inayotia mashaka ya kujiunga na makundi yasiyofaa..

Mini maoni yako juu ya hili tuandikie hapo chini kwenye comment na yatawafikia wahusika moja kwa moja. Endelea kupitia habari mbali mbali hapa simamia.com.