Home Business Vikwazo vya Kibiashara kati ya Tanzania na Zanzibar kutatuliwa.

Vikwazo vya Kibiashara kati ya Tanzania na Zanzibar kutatuliwa.

132
0
SHARE
Muonekano kwa ndani. Jengo la Bunge Zanzibar.
Inaripotiwa kutoka simamia.com na (Shaaban)

Kwa Ufupi: Kumekuwa na Utata wa mda mrefu uliotokana na mfumo mgumu wa uingizwaji wa biashara kati ya Zanzibar na Tanzania Bara.

kisleufahari@gmail.com/simamiateam@gmail.com

Zanzibar: Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salum Ali amesema vikwazo vya kibiashra baina ya Zanzibar na Tazania Bara vinaendelea kufanya mazungumzo na watendaji wa taasisi za Tanzania Bara ili kuondosha vikwazo vya kibiashara baina ya pande hizo mbili.
Hayo ameyasema katika Baraza la Wakilishi Chukwani katika kikao kinachoendelea barazani hapo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayuob aliyetaka kujua, kwanini hivi karibuni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanazinai ilifanya mazungumzo na Serikali ya Kenya kutatua changamoto za kibiashara baina ya nchi hizo na mazungumzo yao yamekuwa ya mafanikio makubwa kwa kupitisha didhaa baina ya Kenya na Tanzania zimetatuliwa .
Je, kwanini kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara kwa mda mrefu kumekuwa na changamoto za wafanyabiashara wa Zanzibar kufanya biashara bila ya bughudha Tanzania Bara licha ya jambo hilo kuwa la muda mrefu bado changamoto hizo zipo kwa miaka mingi zikiwa nchi zao zina udugu wa damu kwa mda mrefu.
Waziri alisema Kenya iliwekea vikwazo Tanazania katika buddhas ya unga na bidhaa ya gesi na hivyo kusababisha usumbufu wa biashara kwa upande wa Tanzania.
Alisema na kwa upande wa Tanzania nayo iliwaekea vikwazo Kenya katika bidhaa za maziwa na sigara kuingia ndani ya soko la Tanzania. Baada ya jambo hilo kupelekwa ngazi za juu viongozi wakuu wa nchi hizo mbili walikubaliana kuondolewa vikwazo baina ya nchi zao mbili na makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano uliofanyika Septemba 8, 2017 mwaka huu.
Alisema kwa upande wa vikwazo vya kibiashara baina Tanzania Bara na Zanzibar, wizara yake inaendelea kufanya mazungumzo na watendaji wa taasisi za bara ili kuondosha vikwazo baina ya nchi hizo mbili.
Waziri huyo amesema hivi karibuni wizara yake ilikuwa na kikao na wizara ya viwanda ili kuangalia matatizo yanayowakabili wafanyabiashara.
Aidha waziri huyo alisema kuwa, kupitia kamati ya kusimamia masuala ya vikwazo vya kibiashara visivyo kuwa vya kiushuru kamati hiyo imeundwa ili kufuatilia changamoto hizo ili hatimaye kuendelea kuzitatua na kuzipatia ufumbuzi muafaka.
Hata hivyo waziri huyo alisema suala la vikwazo vya kibiashara baina yao litazungumzwa kwenye vikao vya mashirikiano baina SMT na SMZ vinavyofuata.

Nini maoni yako tuandikie hapo chini kwenye comment Asante kwa kuendelea kuitembelea simamia.com
Mshirikishe na mwenzako kwa kubonyeza kitufe cha mtandao.