Home Politics Bashe: Magufuli anaakisi mabadiliko

Bashe: Magufuli anaakisi mabadiliko

349
0
SHARE
Mogombea urais kupitia CCm Dk John Magufuli akizungumza na mgombea wa ubunge Jimbo la Nzenga mjini, Hussein Bashe (katikati) na mgombea wa ubunge wa jimbo la Nzega Vijijini, Dk Khamis Kigwangala kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Parking Nzega mjini jana (Picha na Adam Mzee).

MGOMBEA ubunge wa Nzega Mjini kupitia CCM, Hussein Bashe, amesema yeye ni muumini wa mabadiliko ndani ya CCM na kwamba mgombea urais wa chama hicho, Dk John Magufuli ndiye anayeakisi mabadiliko anayotarajia.

Aliyasema hayo jana katika mkutano wa kampeni kwenye jimbo hilo wakati akiomba kuchaguliwa katika nafasi hiyo sambamba na kumpigia kampeni mgombea Urais wa CCM, Dk Magufuli.

Bashe alisema anaamini CCM itabadilika chini ya uenyekiti wa Dk Magufuli na Tanzania itabadilika chini ya Rais Magufuli, kwa kuwa katika kusimamia haki na sheria, mgombea huyo wa CCM hana mchezo.

Alisema kwa kuwa Dk Magufuli amesema ataanzisha Mahakama Maalumu ya Makosa ya Rushwa, akiingia bungeni atamkumbusha Waziri wa Katiba, aeleze lini ataleta muswada wa kuunda mahakama hiyo na kumtaka ianzie bandarini.

Kwa mujibu wa Bashe nchi ina wezi wengi na wengine wako bandarini na baadhi anajua wameanza kutafuta biashara nyingine tangu Dk Magufuli ateuliwe kugombea urais, kwa sababu wanajua hakutakuwa na ukwepaji kodi tena.

Alionya wapinzani kwa siasa za udini, akawataka wamkumbushe mgombea wao (bila kumtaja jina), akalipe fedha za Kanisa la Morovian, alikopeleka hundi feki. Alifafanua kuwa kama watapeleka siasa alizoita za ‘figisufigisu’, basi yeye amekulia ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM, na siasa hizo ndiye mwalimu.